Skip to main content

Yaya Toure kuwaaga mashabiki Etihad Jumanne ya kesho?

Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure (33) huenda akacheza mchezo wake wa mwisho katika dimba la Etihad wakati timu yake ikiwakabili West Bromwich Ablion na hivyo kuwa siku ya kuwaaga mashabiki wa Man City.
Matumaini ya Toure kusalia na Manchester City hayaonikani kutokana na kubakisha wiki chache katika mkataba wake huku kukiwa hakuna maongezi yoyote kati yake na meneja Pep Guardiola juu ya kusaini mkataba mpya.
Toure ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Manchester City amekataa ofa kadhaa za kuachana na klabu hiyo wakati akiwa hana maelewano mazuri na Guardiola lakini inaonekana huenda mechi ya jumanne akaitumia kuwaaga mashabiki kama hali itaendelea kubaki kama sasa.
Katika kipindi cha mwanzo wa msimu, kocha Giardiola aliacha kumchezesha mchezaji huyo mechi kadhaa na zaidi aliacha kumjumuisha katika kikosi ambacho kingeshiriki michuano ya UEFA. Hali hiyo ilimkwaza wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk ambaye alifikia hatua ya kurushiana maneno na Guardiola huku Seluk akisema klabu hiyo itapoteza mashabiki katika bara la Afrika.
Kitendo cha kocha huyo kutompa nafasi kilitafsiriwa kuwa ni mwendelezo kocha huyo wa kuonyesha kuwa Toure halandani na mipango yake kwani akiwa kocha wa Barcelona alimuuza kwenda Manchester City kwa dau la paundi Mil.24 mwaka 2010
Pamoja na hali hiyo Toure alizidi kushikilia msimamo wake wa kutaka kubakia Etihad huku Guardiola akimtaka kumuomba radhi kwa kosa la wakala wake na baada ya muda Toure alimuomba radhi na ndipo alijumuishwa kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya Crystal Palace.

Katika mchezo huo Toure aliwadhihirishia mashabiki kiasi gani kocha alikosea kumuacha kwani aliipatia Man City magoli 2 na kupelekea mashabiki wachache kushangilia hadi kuingia uwanjani.
Kwasasa timu kadhaa zinawinda saini ya kiungo huyo zikiwemo, Westham, Newcastle na Brighton Albion na Inter Milan.
 

Baadhi ya mashabiki wa Manchester City walioingia uwanjani kushangilia na wachezaji wa timu hiyo baada ya Toure kufunga goli la ushindi

Askari wa Uwanjani wakujaribu kuwaondosha mashabiki walioingia uwanjani kushangilia goli la Yaya Toure lililofungwa dk ya 83

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

ABDULRAHMAN MUSA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi April 2017 Katika kinyang'anyiro hicho Mussa amewapiku Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City. Si mara ya kwanza kwa Abdulrahman Mussa kupeba tuzo hii ya uchezaji bora wa mwezi. Katuika msimu wa 2015/2016 Mussa alitajwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Mey 2016 huku akiwapiku wakali kama Donald Ngoma na Ali Nassoro ambapo alicheza michezo mitatu mwezi huo na kufunga magoli 4. Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akipambana na Mshambuliaji wa  Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema. Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme .  Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia. Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana. Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao. Michy Batchuayi akifunga goli 1 na l...