Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema timu yake imejiandaa vizuri na wanamunkari wa hali ya juu wa kutwaa kombe la La Liga msimu huu mbele ya Malaga.
Real Madrid wanawafuata Malaga usiku wa leo katika katika uwanja wa La Rosaleda huku wakihitaji alama moja tu kuwatakatisha kuwa mabingwa wapya wa Laliga 2016/2017.
"Kushinda La Liga sio jambo rahisi na nalijua hilo, tunacheza mechi 38 na unatakiwa kuonyesha nia ya kushinda kila mchezo kwa kila wiki. Wachezaji wamejitahidi na wanastahili kuwa hapo walipo. Wapo kileleni na wanatakuwa kumalizia ligi." aliongeza mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Real Madrid.
Aidha zidane amekimwagia kikosi chake sifa kwa kusema; "Umoja katika timu ndiyo nguzo. Kila mara nimekuwa nikisema, timu inafurahisha kuitazama kwani kila mmoja amekuwa wamuhimu. Ambaye amekuwa hachezi vizuri sana, sasa amekuwa akifanya vyema kama ambaye anayecheza vizuri.Tupo sawa kiakili na kimwili. Tupo vizuri sana."
Madrid watakutana na Malaga inayofundishwa na mchezaji wao (Madrid) wa zamani José Miguel González almaarufu kama "Michel" ambaye siku kadhaa nyuma alikaririwa akisema angependa kuiona timu yake hiyo ya zamani ikitwaa ubingwa maneno yaliyopelekea uvumi kuwa huenda Malaga ikawalegezea Madrid.
Kwa upande mwingine imeonekana kuwa baada ya maneno hayo ya Michel, ambayo yamezua mjadala mkubwa wiki hii hasa upande wa pili wa Barcelona kuwa huenda anataka kuwasaidia Real kupata ubingwa, huenda mchezo huo ukawa mgumu kwa Madrid pale ambapo kocha huyo atataka kudhihirisha kuwa hakumaanisha angewasaidia Madrid kama ilivyotafsiriwa.

Comments
Post a Comment