Imeripotiwa kuwa mshambuliajiwa Borussia Dortmund Piere-Emerick Aubameyang, yupo tayari kuungana na kocha wake wa zamani Jugen Klopp katika kikosi cha Liverpool.
Klopp ndiye aliyemsajili staa huyo mwaka 2013 akitokea St Etienne ya Ufaransa wakati akiifundisha Dortmund.
Aubameyang anayetaka kuondoka Dortmund msimu huu anathaminishwa kwa ada ya kuuzwa, kufikia paundi milioni 61 na endapo Liverpool watatoa kiasi hicho, watainasa saini ya mshambuliaji huyo wa Gabon.
Klopp anahitaji kuimarisha kikosi chake katika dirisha hili la usajili kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa 2017/2018 huku Liverpool ikikabiliwa na michuano ya UEFA endapo watafuzu hatua ya mtuano.
Tangu kuondoka kwa Luis Suarez, Liverpool haijapata mshambuliaji (Goal Machine) mwenye uwezo wa kuihakikishia Liverpool magoli zaidi ya 20 hasa baada Daniel Sturrige kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Usajili wa Mario Baloteli, Paul Lambert na Christian Benteke haukufua dafu kwa washambuliaji hao kushindwa kufunga hata magoli 15 kwa msimu.
Wiki chache zilizopita Rada Yetu tuliripoti taarifa ya Aubameyang kukubali kujiunga na PSG ila dili hilo halikufanikiwa baada ya miamba hiyo ya Ufaransa kuachana na nyota huyo huku kocha wao Unai Emery akisisitiza kuwa Edson Cavani anatosha.
Aubameyang ameweka rekodi nzuri ya ufungaji katika klabu ya Dortmund tangu alipojiunga akifunga jumla ya magoli 120 kati ya mechi 189. Katika msimu uliopita ameifungia Dortmund magoli 31 katika mechi 32 na kubeba tuzo ya ufungaji bora wa Bundersliga
Na Walter Steven

Comments
Post a Comment