Kiungo wa West Ham na timu ya taifa ya Norway Havard Nordtveit amesajiliwa na klabu ya Hoffenheim inayoshiriki ligi ya Bundersliga, Ujerumani.
Mnorway huyo (27) aliyewahi pia kuitumikia Arsena, amekamilisha kujiunga na klabu hiyo kwa ada ambayo bado haijawekwa wazi.
Kuuzwa kwa Norditveit kwenye klabu hiyo kunamfanya arejee ujerumani katika ligi aliyoizoea kwani awali West Ham walimsajili akitokea Borussia Monchengladbach msimu uliopita.
Tangu asajiliwe na wagonga nyundo hao wa London, Norditveit amefanikiwa kuingia uwanjani mara 21tu, na kati ya hiyo 15 ikiwa ni ya ligi lakini hajafunga goli hata moja.
Hoffenheim imemaliza katika nafasi ya nne(4) katika msimamo wa Bundesliga na hivyo kuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao.
Kocha wa timu hiyo Julian Nagelsman na kikosi chake, kitacheza mechi za hatua ya mtoano kabla ya kufuzu kushiriki michuano hiyo ya Ulaya na hivyo anahitaji kuimarisha kikosi chake ili waweze kushinda michezo hiyo na kufuzu UEFA rasmi.

Comments
Post a Comment