Jose Mourinho akiwa na marehemu baba yake, Jose Manuel Mourinho Felix mwaka 2003 |
Mzee Mourinho amefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 79. Katika maisha yake ya soka Mourinho amewahi kuzitumikia klabu mbili kubwa za Ureno ambazo ni Victoria Setubal na Belenenses.
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameposti
Mourinho alikuwa akicheza nafasi ya mlinda mlango katika klabu hizo ambapo ameichezea Victoria Setubal tangu 1955–1968 akicheza mechi 143 na Belenenses tangu 1968–1974 akicheza michezo 131.
Tofauti na maisha ya uchezaji, Mourinho amewahi pia kuvifundisha vilabu vingi vya Ureno vikiwemo vyote alivyochezea pamoja na Rio Ave, Caldas, Amora, Valzim, Madeira, Leiria, O Elvas na Estrela Portalegre.
Kwa mujibu wa ripoti mbali mbali, mkongwe huyo atazikwa kwao nchini Ureno siku ya kesho.
Comments
Post a Comment