Na Walter Stephan.
Olympic Lyon imefanikiwa kumsajili mlinzi wa pembeni kutoka Benfica Fernando Marcal kwa ada ya Euro milioni 4.5
Marcal mwenye miaka 28 amemaliza msimu uliopita katika ligi ya Ufaransa alipokuwa akiitumikia Guingamp kwa mkopo akitokea Benfica.
Pamoja na kucheza katika nafasi ya ulinzi, Mbrazili huyu amejizolea sifa kutikana na uwezo wake wa kutoa pasi za mwisho. Kwa msimu uliopita Marcal ametoa jumla ya pasi 7 zilizozaa magoli katika michezo 31 aliyoanza na klabu hiyo ya Ufaransa ambao ni mahasimu wa Lyon.
Marcal ni zao la klabu ya Gremio ya Brazil na amepitia timu kadhaa zikiwemo Guaratinguetá,Torreense, na baadae Nacional ya Ureno kabla ya kusajiliwa na Benfica 2015.
Katika klabu ya Benfica, Marcal hakufanikiwa kupata nafasi na alitolewa kwa mkopo Gaziantepspor ya Uturuki kwa msimu wa 2015-2016 na baadae Guingamp 2016-2017.
Comments
Post a Comment