Leicester City imefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi kutoka Hull City Harry Maguire (24) kwa ofa ya paundi Milioni 17.
Maguire amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Leicester ambao walikuiwa mabingwa wa mwaka jana.
Baada ya kumwaga wino King Power, Maguire alikuwa na haya yakusema:
"Ni vilabu vingi vimekuwa vikinihitaji lakini baada ya kukutana na Kocha wa hapa (Leicester) ameonekana kubebana vizuri sana na uelekeo wa klabu. Leicester inakuja juu na inaonyesha mwelekeo mzuri kwa siku za usoni".
Dili hili linatarajiwa kuinufaisha pia Sheffield United ambayo ni timu ya zamani ya mlinzi huyo kutokana na makubaliano ya kwenye mkataba wa kuuzwa kwake ambapo, Sheffield watanufaika kwa asilimia 10%
Maguire anaenda kugombania namba na mabeki wawili wa kati ambao ni Wes Morgan na Robert Huth waliofanikiwa kuunda ukuta mgumu kwa wapinzani kuupenya hapo Leicester.
Hata hivyo ni kutokana na ya majeruhi inayowakabili wawili hao, hususani Morgan, ndiyo chachu iliyowapekea "Foxes" kuingia sokoni.
Hata hivyo ni kutokana na ya majeruhi inayowakabili wawili hao, hususani Morgan, ndiyo chachu iliyowapekea "Foxes" kuingia sokoni.
Comments
Post a Comment