Olympic Marseille inatarajiwa kukamilisha usajili wa Valere Germain kutoka kwa mabingwa wa Ufaransa AS Monaco.
Germain ambaye kipaji chake kimekuzwa na timu ya vijana ya Monaco B alianza kuitumikia timu ya wakubwa mwaka 2011 na mpaka sasa ameichezea Monaco mechi 159 na kufunga jumla ya magoli 41.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 sasa ameisaidia timu yake ya Monaco kutwaa ubingwa wa msimu uliopita 2016/2017 baada ya kurejea katika kikosi hicho cha Leonardo Jardim akitokea timu ya Nice ya ligi hiyo aliyoitumikia kwa mkopo ambako alipachika jumla ya magoli 14 katika mechi 38.
Kwa msimu huu uliomalizika Germain ameifungia Monaco jumla ya Magoli 10 katika michezo 27 ya ligi aliyoshuka dimbani (jumla magoli 14 katika michezo yote 36) na kuisaidia pia kutinga hadi hatua ya nusu fainali ya ligi ya magingwa UEFA.
Dau la Euro milioni 8 linasemekana kukubaliwa kwa steika huyo aliyeshindwa kutamba mbele ya Kylian Mbappe na Radamel Falcao.
Comments
Post a Comment