Mashabiki wa Manchester City wameibuka ghafla kwenye mitandao mchana huu kwa ghadhabu baada ya mchezaji wao Nicolas Otamendi kumjeruhi Gabriel Jesus katika mchezo wa kimataifa baina ya timu hizo.
Otamendi na Jesus wote wanatokea klabu moja ya Machester City na walikutana masaa machache leo katika mchezo uliomalizika kwa Argentina kushinda kwa goli 1-0.
Otamendi alimgonga Jesus maeneo ya usoni aliporuka akitokea nyuma ya mchezaji huyo wa Brazil kuwania mpira wa juu na kupelekea Jesus kutolewa nje na machela.
Hali hiyo imeonekana kuwakera mashabiki wa Manchester City hali ilioyojidhihirisha kwenye mitandao ya kijamii kwa beki huyo kukosa umakini na kumjeruhi mwenzake.
Wengine wamefikia hatua ya kumtaka kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola amuuze beki huyo pindi tu atakaporejea klabuni hapo.
Jesus akitolewa nje ya uwanja kwa Machela baada ya kuumizwa na mchezaji mwenzake wa Man City Nicolas Otamendi |
Comments
Post a Comment