Cristiano Ronaldo akiwa na Kocha wake wa zamani Sir. Alex Ferguson baada ya kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya fainali ya UEFA. |
Habari hii imeanza kuonekana kuleta mabadiliko kwa Manchester United kwani mpaka sasa wameonekana kusitisha mipango yao mingine ya usajili.
Man U walikuwa katika hatua nzuri ya kumuwania Alvaro Morata kutoka hapo hapo Madrid na ilisemekana usajili huo ungekamilika msimu huu na mchezaji huyo kufanya vipimo vya afya. Baada ya tetesi za Ronaldo kutaka kurejea katika klabu hiyo, kumezima habari hizo za Morata huku, mapema leo hii habari zikisema kuwa Chelsea wako mbioni kuteka usajili wa Staa huyo.
Mfululizo wa habari kumhusu Ronaldo umeenda mbali zaidi baada ya jarida la Marca kuripoti kuwa Ronaldo amemtaka wakala wake Jorge Mendes kuhakikisha anafanikisha kumrejesha Old Trafford.
Ronaldo amefikia hatua hiyo baada ya kuripotiwa kuwa hajihisi mwenye furaha katika kikosi cha kocha Zidane. Inasemekana pia kuwa mashabiki wa Madrid wameanza kudai kutoridhishwa na kiwango cha staa huyo Mreno.
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir. Alex Ferguson amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na Ronaldo na huenda akawa amehusika kwa kiasi kikubwa katika kumshawishi Ronaldo ili arejee Manchester.
Ferguson alionekana pia katika fainali ya UEFA akisalimiana na staa huyo hata kufikia kupiga nae picha
Comments
Post a Comment