Ripoti zinasema kuwa Salah anatarajiwa kusaini mkataba na klabu ya Liverpool baada ya Liverpool kufikia dau la Euro milioni 40 pamoja na nyongeza ya Euro mil. 5 ambapo jumla yake ni sawa na Paundi milioni 39.5.
Kwamujibu wa mwaandishi wa habari Hady Elmedany, Salah anatarajiwa kutua katika jiji la London akitokea Cairo majira ya saa 3:05 usiku.
Liverpool imekuwa ikimuwania Salah tangu kumalizika kwa ligi kuu mwezi May huku baadhi ya ofa zao zikikataliwa na Roma mara kadhaa, pamoja na Salah kuwa tayari kutua Anfield.
Comments
Post a Comment