Mchezaji wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry (21) amesajiliwa na miamba ya Ujerumani Bayern Munich.
Gnabry mwenye miaka 21 amejiunga na Bayern akitokea klabu ya Werder Bremen aliyojiunga nayo mwaka jana 2016. Katika muda mfupi alioitumikia Bremen Gnabry ameonyesha uwezo mkubwa kwa kufunga magoli 11katika mechi 27 huku akitokea sehemu ya pembeni mwa uwanja yaani akicheza kama kiungo mshambuliaji (Winga).
Baada ya kukamilika kwa uhamisho huo Gnabry amesema kuwa "Ni heshima sana kuwa sehemu ya Bayern FC. Mbele yangu naona mambo mazuri nikiwa na Bayern na natizama mbele kushuhudia hayo." Alisema Gnaby.
Gnaby aliuzwa na Arsenal mwaka 2016 kuelekea Werder Bremen baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Arsene Wenger.
Kabla ya kuuzwa kwenda Werder Bremen, Gnabry alitolewa kwa mkopo kwenda West Bromwich msimu wa 2015/2016 ambako alicheza mechi moja tu na baada ya msimu kuisha alirejea Arsenal na ndipo Wenger alipoamua kumtoa kwa timu hiyo ya Ujerumani.
Gnabry mwenye miaka 21 amejiunga na Bayern akitokea klabu ya Werder Bremen aliyojiunga nayo mwaka jana 2016. Katika muda mfupi alioitumikia Bremen Gnabry ameonyesha uwezo mkubwa kwa kufunga magoli 11katika mechi 27 huku akitokea sehemu ya pembeni mwa uwanja yaani akicheza kama kiungo mshambuliaji (Winga).
Baada ya kukamilika kwa uhamisho huo Gnabry amesema kuwa "Ni heshima sana kuwa sehemu ya Bayern FC. Mbele yangu naona mambo mazuri nikiwa na Bayern na natizama mbele kushuhudia hayo." Alisema Gnaby.
Gnaby aliuzwa na Arsenal mwaka 2016 kuelekea Werder Bremen baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Arsene Wenger.
Serge Gnabry akiwa akizini akiitumikia Werder Bremen |
Comments
Post a Comment