Aliyekuwa nahodha wa Chelsea John Terry amesajiliwa na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi ya Championship.
Terry aliyeachana na Chelsea mwishoni mwa msimu ulioisha May 2017 amesajiliwa na Aston Villa akiwa ni mchezaji huru.
Villa kupitia tovuti yao leo, wamethibitisha kukamilisha usajili wa beki huyo mzoefu. Terry ameitumikia Chelsea kwa miaka 19 tangu 1998 akiichezea jumla ya michezo 717. Kati ya hiyo amecheza michezo ya ligi 492 kufunga magoli 41.
Terry ni mmoja kati ya wachezaji watatu waliocheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Chelsea, akiongozwa na Ron Harris (791) na Peter Bonetti (729)

Comments
Post a Comment