Beki wa Mfaransa Gael Clichy ametimkia katika kikosi cha Istanbul Basaksehir ya Uturuki bure baada ya kuachana na Manchester City iliyokataa kumuongezea mkataba.
Clichy aliachiwa huru mapema mwishoni mwa mwezi May akiwa pamoja na wenzake wanne ambao ni Sagna, Zabaleta, Caballero na Navas.
Basaksehir imethibitisha taarifa za usajili huo kupitia ukurasa wao wa twitter, huku taarifa zinazoaminika zikisema kuwa nyota huyo amekubaliana na ofa ya paundi milioni 2.5 kwa msimu.
Beki huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya ijumaa ya leo nchini humo, tayari kwa kuanza kandarasi mpya ambayo kwamujibu wa klabu hiyo, Clichy atasaini mkataba wa miaka mitatu.
Clichy mwenye umri wa miaka 31 sasa, alihamia Manchester City akitokea Arsenal mwaka 2013 na ameichezea City jumla ya michezo 192.
NYINGINE:

Comments
Post a Comment