Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Olympic Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa Alexandre Lacazette kwa ada ya paundi milioni 46.5.
Uhamisho huo umeenda sambamba na kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Arsenal huku washika mitutu hao wa London wakikuvunja rekodi ya awali ya usajili iliyokuwa ikishikiliwa na Mesut Ozil aliyenunuliwa kwa paundi mil. 42 akitokea Real Madrid 2013.
Lacazette mwenye miaka 26 ameweka ukomo wa miaka 14 aliyodumu katika klabu ya Lyon ambapo ameifungia magoli 100 ya ligi katika michezo 203 na katika misimu miwili ya mwisho ameifungia Lyon magoli zaidi ya 30 katika michezo yote.
NYINGINE: Pepe akamilisha usajili wa kuhamia Besiktas
Awali Lacazette alikwishafikia makubaliano ya awali na Athletico Madrid tayari kwa kujiunga na klabu hiyo, ila uhamisho huo ukafeli baada ya klabu hiyo kufungiwa kufanya usajili msimu huu.

Comments
Post a Comment