Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya Everton juu ya kumsajili mshambiliaji wao Romelu Lukaku kwa ada ya paundi mil 75
Lukaku aliyefunga magoli 25 msimu uliopita aliweka wazi mapema kuwa hatosalia katika kikosi cha Everton na angetaka kujiunga na timu inayoshiriki michuano ya mabingwa Ulaya UEFA.
Lukaku mwenye miaka 24 sasa, amefikia makubaliano na Manchester United baada ya klabu hiyo kuachana na Zlatan Ibrahimovic na anatajwa kuwa mbadala wake pale Old Traford.
Awali Lukaku alihusishwa na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Chelsea mapema baada ya ligi kumalizika, kabla ya kuja kwa ukimya tetesi hizo kupotea.
Kinachosubiriwa sasa ni endapo Lukaku atapata nafasi ya kudumu katika kikosi hicho cha Jose Mourinho huku kocha huyo akiwa ndiye aliyemwacha awali na kutimkia Everton 2014.
NYINGINE: Lacazette amejiunga rasmi na klabu ya Arsenal

Comments
Post a Comment