Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan amesajiliwa ma klabu ya Kayserispor ya Uturuki akitokea Shanghai SIPG ya China.
Nyota huyo wa Ghana ambaye ndiye Mwafrica anayeongoza kwa magoli katika Kombe la Dunia (magoli 6) ametokea katika klabu ya Al Ahli Dubai aliyokuwa akiitumikia kwa mkopo.
Gyan atapokea kitita cha Euro milioni 1.5 kwa mwaka katika kandarasi yake na klabu hiyo ya Kayserispor maarufu kama Anatolian Stars.
Hii ni mara nyingine tena kwa Gyan kurejea katika bara la Ulaya tangu mara ya mwisho 2011 alipoondoka Sunderland kwa mkopo kwenda Al Ain na kisha kuhama moja kwa moja katika klabu hiyo ambapo ni miaka 6 mpaka sasa.
Anakumbukwa kwa kiwango kizuri alichoonyesha akiwa Sunderland na mshambuliaji mwenzake Darren Bent, huku akibeba tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa Afrika 2010.
Kuna uwezekano wa Gyan kukutana tena na Bent katika ligi hiyo ya Super League,kwani mshambuliaji huyo anayeichezea Derby Country kwasasa, amekuwa akihusishwa kujiunga na Sivasspor.
NYINGINE:

Comments
Post a Comment