Sandro Ramirez akitia saini Mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Everton |
Everton kuamkia leo wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Sandro Ramirez kutoka Malaga pamoja na mlizi Michael Keane kutoka Burnley.
Sandro amesajiliwa kwa ada ya paundi milioni 5.25 na amesaini mkataba utakaomuweka Goodson Park kwa miaka mitatu.
Kwa upande wake Keane yeye amesajiliwa kwa ada ya paundi mil.30 akitokea Burnley na amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu hiyo
Wawili hao wameungana na Jordan Pickford (kipa), Davy Klaassen (kiungo) na Henry Onyekuru (straika) ambao wameshatua Goodson Park.
Kuthihirisha kuwa Everton inayonolewa na kocha anayeshikilia rekodi ya beki aliyefunga magoli mengi zaidi Ronald Koeman, imejipanga vizuri kwenye usajili huu, Kwasasa wanataka kumrudisha Staa wa Manchester United Wayne Rooney katika timu hiyo aliyokulia.
Nyinginezo: John Terry atimkia Aston Villa
Inadaiwa pia klabu hiyo (Everton) inafikiria kutupa karata kwa mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud na huenda wakafanikliwa endapo Arsenal watapata saini ya Alexandre Lacazette.
Beki Michael Keane akiwa amepoz pembeni ya nembo ya klabu ya Everton baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano |
Comments
Post a Comment