Timu ya Everton ipo njiani kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Malaga Sandro Ramirez kwa ada ya paundi milioni 5
Ramirez ameonekana na kupigwa picha akiwasili katika jiji la Liverpool ambapo ipo klabu hiyo ya Everton akisemekana kwenda kukamilisha usajili huo.
Kocha wa Everton Ronald Koeman amekuwa akiwania saini ya mshambuliaji huyo tangu kumalizika kwa msimu wa ligi mwezi May.
Sandro mwenye umri wa miaka 21 (atatimiza miaka 22 mwezi ujao) ni zao la Catalunia akitoka timu ya vijana ya Barcelona aliyoitumikia tangu 2013 kabla ya kupandishwa tumu ya wakubwa 2014/2015 alipoichezea michezo 17 na kufunga magoli 2. Mwaka 2016 alitimka Barcelona na kuhamia Malaga na endapo uhamisho huu utakamilika, atakuwa ameitumikia Malaga kwa msimu mmoja tu mpaka sasa.
Ujio wa Sandro unahitajika sana na Everton kufuatia hatihati ya kuondoka kwa mshambuliaji wao tegemezi Romelu Lukaku ambaye ameshaweka wazi kuwa hatosalia katika kikosi hicho cha Merseyside huku Chelsea ikiwa imeonesha nia ya kumrejesha stanford Bridge
Everton pia inakaribia kumnasa nahodha wa Ajax Davy Klaassen mwenye umri wa miaka 24 ikiwa ni mipango ya Koeman kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao

Comments
Post a Comment