Skip to main content

Ratiba nzima ya Arsenal msimu wa Premier League 2017/2018

The Gunners wataanza msimu kwa kuwakaribisha mabingwa wa mwaka jana Leicester City katika uwanja wao wa Emirates.
Arsenal ambao kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 21 wameshindwa kumaliza ligi katika nafasi nne za juu, watahitaji kuzichanga vyema karata zao ili kurejea kwenye makali huku Kocha Arsene Wenger akionekana kuwa bize kwenye usajili huu, huku akiwa tayari ameshaanza kusajili kwa kumsajili beki Kolasinac kutoka Shalke04.
Ndani ya mwezi huohuo wa August, Arsenal watakutana na Liverpool, waliowapokonya nafasi ya nne na pengine wakatumia mchezo huo ambao ndio mechi kubwa ya kwanza, kuonyesha namna walivyojipanga msimu huu.
Liverpool iliwafunga Arsena katika michezo yote miwili ya ligi kuu msimu uliopita, huku wakigombania nafasi ya nne katika mechi za lala salama.
Ungwe ya mwisho itawashuhudia washika mitutu hao wakiwa ugenini kuwakabili Huddersfield Town waliopanda daraja.
TAREHEMUDA MECHI
12/08/2017 15:00 Arsenal v Leicester City
19/08/2017 15:00 Stoke City v Arsenal
26/08/2017 15:00 Liverpool v Arsenal
09/09/2017 15:00 Arsenal v Bournemouth
16/09/2017 15:00 Chelsea v Arsenal
23/09/2017 15:00 Arsenal v West Bromwich Albion
30/09/2017 15:00 Arsenal v Brighton and Hove Albion
14/10/2017 15:00 Watford v Arsenal
21/10/2017 15:00 Everton v Arsenal
28/10/2017 15:00 Arsenal v Swansea City
04/11/2017 15:00 Manchester City v Arsenal
18/11/2017 15:00 Arsenal v Tottenham Hotspur
25/11/2017 15:00 Burnley v Arsenal
28/11/2017 19:45 Arsenal v Huddersfield Town
02/12/2017 15:00 Arsenal v Manchester United
09/12/2017 15:00 Southampton v Arsenal
12/12/2017 19:45 West Ham United v Arsenal
16/12/2017 15:00 Arsenal v Newcastle United
23/12/2017 15:00 Arsenal v Liverpool
26/12/2017 15:00 Crystal Palace v Arsenal
30/12/2017 15:00 West Bromwich Albion v Arsenal
01/01/2018 15:00 Arsenal v Chelsea
13/01/2018 15:00 Bournemouth v Arsenal
20/01/2018 15:00 Arsenal v Crystal Palace
30/01/2018 19:45 Swansea City v Arsenal
03/02/2018 15:00 Arsenal v Everton
10/02/2018 15:00 Tottenham Hotspur v Arsenal
24/02/2018 15:00 Arsenal v Manchester City
03/03/2018 15:00 Brighton and Hove Albion v Arsenal
10/03/2018 15:00 Arsenal v Watford
17/03/2018 15:00 Leicester City v Arsenal
31/03/2018 15:00 Arsenal v Stoke City
07/04/2018 15:00 Arsenal v Southampton
14/04/2018 15:00 Newcastle United v Arsenal
21/04/2018 15:00 Arsenal v West Ham United
28/04/2018 15:00 Manchester United v Arsenal
05/05/2018 15:00 Arsenal v Burnley
13/05/2018 15:00 Huddersfield Town v Arsenal

Comments

Popular posts from this blog

Wajue Wafungaji bora wa EPL kwa kila timu inayoshiriki sasa

1. CHELSEA - Frank Lampard -147 Lampard ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa Chelsea wa muda wote yaani tangu (Chelsea) ilipoanzishwa akitupia kambani magoli 211. Alisajiliwa akitokea West ham mwaka 2001 na kwa sasa ni moja kati ya mashujaa wa kubwa wa klabu ya Chelsea. Alifunga goli la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea December 23, 2001. Goli la mwisho alilifunga 05 April 2014. 2. TOTTENHAM - Teddy Sheringham - 98 Teddy Sheringham anafahamika kama "Legend" wa Tottenham Hotspurs pamoja na kuvichezea vilabu takribani 10 vya nchini uingereza ikiwemo Manchester United na West ham United. Alisajiliwa na Tottenham akitokea Nottingham Forest mwaka 1992 na alisajiliwa na Man United 1997 kabla ya kurejea tena Tottenham 2001. Aliifungia Spurs goli la kwanza tar.02.september 1992 na la mwisho tar. 21 April 2003 kabla hajatimkia Portsmouth   3. MANCHESTER CITY - Sergio Aguero -120 Akiwa amesaliwa na magoli 10 tu kuwa mfungaji bora wa historia wa M...

ABDULRAHMAN MUSA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi April 2017 Katika kinyang'anyiro hicho Mussa amewapiku Jafar Salum wa Mtibwa Sugar na Zahoro Pazi wa Mbeya City. Si mara ya kwanza kwa Abdulrahman Mussa kupeba tuzo hii ya uchezaji bora wa mwezi. Katuika msimu wa 2015/2016 Mussa alitajwa tena kuwa mchezaji bora wa ligi kuu mwezi Mey 2016 huku akiwapiku wakali kama Donald Ngoma na Ali Nassoro ambapo alicheza michezo mitatu mwezi huo na kufunga magoli 4. Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akipambana na Mshambuliaji wa  Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim

Chelsea Mabingwa Wapya EPL 2016/2017

Michy Batchuayi apeleka shangwe kwa wapenzi wa "The Blue". Alazimisha sherehe ianze mapema. Sasa kurejea Stamford Bridge, Watford wakiwapoke kwa makofi kama wafalme .  Chelsea wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Uingereza, England Premier League baada ya kujikusanyia pointi ambazo hakuna timu yoyote kwasasa inayoweza kuzifikia. Mbelgiji Michy Batchuay ndie aliyelazimisha Chelsea kupewa tiketi ya kuanza kusherekea ubingwa wao baada ya kuipatia chelsea bao pekee dk ya 82 akiteleza kumalizia pasi iliyoingizwa na  Cesar Azpilicueta katika mchezo ulioonekana kuwa mgumu sana. Batchuayi alitokea benji akichukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika mabadiliko mawili ya utata yaliowashangaza mashabiki wa Chelsea ambapo Eden Hazard naye alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Willian. Baada ya mabadiliko haya Chelsea walianza kushambuliwa lakini ukuta wao ukiongozwa na Cahil, Luiz na Azpilicueta uliweza kuimili vishindo vya wenyeji wao. Michy Batchuayi akifunga goli 1 na l...