Ripoti zinasema kuwa kiungo wa Chelsea Eden Hazard amezungumza na rafiki zake na kuwaambia kuwa anataka kujiunga na real Madeid ili kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia. Kiungo huyo wa ubelgiji amekuwa katika rada ya Real Madrid baada ya kuwa katika kiwango kizuri kwa misimu kadhaa sasa akiwa na ‘the Blues’. Mara kadhaa Hazard amekuwa akitoa kauli zisizoonyesha hasa uelekeo wake ni upi baada ya kumalizika kwa msimu huu, japokuwa kwa mujibu wa mkataba wake mpaka sasa, Hazard ana muda wa miaka 3 ya kuitumikia Chelsea. Alipowahi kuuulizwa kuhusu hatima yake, Hazard amesema “Suala hilo halipo kwenye akili yangu kwa sasa. Nachojua ni kwamba nina miaka 2 au 3 iliyobaki katika mkataba wangu. Nahitaji kumaliza msimu na kisha tutajua nini kinaendelea". Katika hatua nyingine taarifa zinasema kuwa uongozi wa klabu ya Chelsea upo katika harakati za kumuita mezani Hazard kwa mazungumzo ya kumpati a mkataba mwingine.