Gylfi Sigurdsson anatarajiwa kusajiliwa na Everton muda wowote toka sasa kufuatia taarifa kuwa Everton wamekubaliana na klabu yake ya Swansea City kuhusu uhamisho huo. Sirgudsson ambaye ni kiungo mshambuliaji wa kati wa Swansea amekuwa na kiwango kizuri tangu ahamie klabuni hapo akitokea Tottenham mwaka 2014. Uwezo wake wa kucheza katika nafasi zaidi ya moja na umaarufu wake katika kupiga mipira iliyokufa nje ya 18 (free-kick) umemfanya kuwa mmoja wa viungo bora na kupelekea kuwa mmoja kati ya wachezaji waliohitajika na Ronald Koeman mapema baada ya ligi kuu kumalizika. Endapo usajili wa Rooney utakamilika mapema, basi Gylfi Sirgudsson utakuwa ni mchezaji wa nane kujiunga na Everton katika dirisha hili la usajili.