Klabu ya FC Bournemouth imemsajili kipa Asmir Begovic kutoka Chelsea kwa ada ambayo bado halijawekwa wazi mpaka sasa. Chelsea ilimsajili Begovic kutoka Stoke City alikoitumikia kwa mafanikio kwa kucheza jumla ya mechi 160 huku pamoja na kucheza nafasi hiyo, alibahatika kuifungia Stoke goli moja ambalo ndio pekee katika michezo 259 aliyoshuka uwanjani na vilabu mbali mbali. Begovic (29) anaenda kuitumikia Bournemouth kwa mara ya pili akiwa ameshawahi kuichezea kwa mkopo akitokea klabu ya Portsmouth mwaka 2007. Pamoja na dau hilo kutowekwa wazi, inasemekana kuwa Begovic ameuzwa kwa ada ya paundi mil.10 huku tayari Chelsea ikiwa imeanza mbio za kumuwania mlinzi wa PSG Alphonse Areola (24) ili kuziba pengo la Begovic. Begovic ameichezea chelsea jumla ya mechi 19, tangu aliposajiliwa akitokea Stoke, huku akishindwa kujiimarisha kama kipa namba moja wa chelsea kutokana na chaguo la kwanza kuwa ni mbelgiji Thibaut Courtois. Baada ya kukamilisha usajili huo, mlinzi huyo kutoka Bosnia ...