Enzo Zidane akielekezwa jambo na baba yake Zinadine Zidane akiwa Real Madrid. Klabu ya Alaves imemsajili Enzo Zidane mtoto wa kocha wa Real Madrid Zinadine Zidane na atasaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo ya La Liga. Enzo mwenye miaka 22, ameruhusiwa kuondoka na baba yake (Zidane) baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza. Anaondoka Real Madrid akiwa amefanikiwa kuifungia goli moja tu katika mechi ya Copa del Rey dhidi ya Leonesa katika ushindi wa magoli 6-1. Enzo amekulia Madrid tangu utoto wake na kuondoka kwake kunatazamiwa kuwa ni njia ya kumpa nafasi ya kupata uzoefu zaidi kwa kumtafutia timu ambayo huenda akapata nafasi ya kuonyesha kiwango chake.